KIMBUNGA CHASABABISHA SAFARI KUAHIRISHWA JAPAN

 

Safari za ndege zaidi ya 500 zimefutwa katika viwanja vya ndege vya nchini JAPAN baada ya kimbunga chenye nguvu cha VONGFONG kupiga katika visiwa vikuu vya nchi hiyo leo.
Kimbunga hicho kilichoambatana na mvua kubwa kimesababisha maelefu ya watu watu kuyahama makazi yao na wengine kukesha katika viwanja vya ndege na gari moshi baada ya huduma hizo kusitishwa.

Mtu mmoja ameripotiwa kupotea na wengine 56 kujeruhiwa katika maeneo ya visiwa vilivyokumbwa na kimbunga hicho cha kimbunga VONGFONG.

Wakala wa hali ya hewa wa JAPAN wamesema upepo uliokuwa ukisafiri kwa kasi ya kilomita 180 kwa saa ulitua katika eneo la MAKARUZAKI kwenye kisiwa cha KYUSHU asubuhi ya leo.

Kimbunga hicho cha 19 kwa msimu huu tayari kilikishambulia kisiwa cha OKINAWA Kusini-Mashariki mwa JAPAN mwishoni mwa wiki