KIONGOZI WA BOKO HARAM AKANUSHA KUUAWA

Kiongozi wa Boko Haramu Abubakr Shekau  akanusha kuuawa.
Kiongozi wa Boko Haramu Abubakr Shekau akanusha kuuawa.
Hatimaye kiongozi wa Boko Haram aibuka toka mafichoni na kukanusha habari zilizoenea kwamba aliuawa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita. Katika Kanda ya video inayomuonyesha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram imetolewa akikana madai ya jeshi kwamba amefariki.
Aidha, katika kanda hiyo, Abubakr Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita. Wiki iliyopita jeshi lilidai kuwa mtu anayejionyesha katika kanda ya video ya Boko Haram aliuawa na mwezi Agosti 2013 likadai kwamba huenda Shekue amefariki.
Mwandishi wa Nigeria Ahmad Salkida ,ambaye ana mawasiliano mazuri na Boko Haram alisema kuwa katika mtandao wake wa Twitter wiki iliopita ana hakika kwamba Shekue yu buheri wa afya na kwamba hajafariki.
Kwa upande mwingine katika kanda hiyo ya video mtu aliyezungumza katika kanda hiyo alikuwa Abubakr Shekue yule yule anayeonekana katika kanda nyingine za video za kundi la Boko Haram.