HII ni Dabi ya Jiji la London na hii ni moja ya Mechi kubwa za Msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu England wakati Stamford Bridge itakapo waka moto Jumapili kwa Mechi kati ya Chelsea na Arsenal.
Jose Mourinho atatinga kw
enye Mechi hii akiwa na imani kubwa kwani wako kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Arsene Wenger Arsenal ambao wako Nafasi ya 5.
Kwenye Mechi kama hii Msimu uliopita iliyochezwa Mwezi Machi Arsenal walibondwa 6-0 na Chelsea baada ya kuongoza 2-0 na kisha Arsenal kupata pigo la Fulbeki wao Kieran Gibbs kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hali za Wachezaji
Chelsea

Ingawa Mourinho hivi karibuni aliungama Straika wake Diego Costa hawezi kucheza Mechi mbili mfululizo ndani ya Wiki kutokana na maumivu ya Musuli za Pajani na kati ya Wiki aliichezea Chelsea ilipocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, lakini itashangaza mno ikiwa Costa hatacheza Mechi hii ukizingatia ukubwa wake.
Arsenal
Listi ya Majeruhi wa Arsenal ni ndefu.
Wapo Mathieu Debuchy, Nacho Monreal, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Olivier Giroud na Yaya Sanogo.
Ingawa Theo Walcott ameshapona Goti lake alilofanyiwa operesheni mwanzoni mwa Mwaka lakini hajawa fiti kucheza Mechi.
Vikosi vinatarajiwa:
CHELSEA: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Costa
ARSENAL: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere, Sanchez, Ozil, Oxlade-Chamberlain, Welbeck
REFA: Martin Atkinson