MKE WA MUGABE AWAASA MAAFISA WA ZANU-PF KUFUATA MISINGI YA MUGABE

GRACE MUGABE


Mke wa Rais ROBERT MUGABE wa ZIMBABWE, GRACE MUGABE, ametoa wito kwa maafisa wa chama kinachotawala nchini humo, cha ZANU-PF, kuzingatia misingi na kanuni za Rais MUGABE na kueleza kwamba KATU, ZIMBABWE haitapata kiongozi mwingine BORA kama MUGABE. 

Akifungua mkutano wa wafuasi wa ZANU-PF kufuatia kuteuliwa kwake kuongoza Umoja wa Wanawake wa chama hicho, GRACE MUGABE pia amewashutumu viongozi wa ngaz za juu wa chama hicho kwa kuwa NA njama za kumpindua mumewe, Rais MUGABE. 

GRACE MUGABE amedai kwamba wengi wa maafisa wa juu wa chama cha ZANU-PF hawana sifa za kukiongoza chama hicho na kwamba MUGABE ndiye pekee mwenye dira ya kukiongoza vyema chama cha ZANU-PF na nchi hiyo . 

Amewataka wananchi wa ZIMBABWE kuendelea kumuunga mkono Rais MUGABE na kumpigia kura katika uchaguzi mkuu ujao akieleza kwamba MUGABE ni kiongozi bora asiye kuwa na tamaa ya kujitajirisha nchini humo.