MKURUGENZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA AMEFUNGUA SEMINA YA UJASIRIAMALI YA SIKU TATU HII LEO CHUONI HAPO.

Mkurugenzi wa chuo chuo cha uandishi habari na utangazaji Arusha bwana Joseph Mayagila amefungua semina ya siku tatu ya ujasiriamali leo itakayomalizika siku ya ijumaa chuoni hapo.
pichani ni; Mkurugenzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Joseph Mayagila

Bwana Joseph Mayagila amesema kuwa semina hiyo ni muhimu sana kwa wanafunzi wote kwa sababu dunia ya sasa imejengeka katika misingi ya ujasiriamali.

Alisema kuwa ili mtu yeyote afanikiwe kibiashara ni lazima ajue kupanda mbegu, thamani ya muda pamoja na mavuno ambayo ni matokeo ya kupanda mbegu.

“Unaweza kuhangaika sana kwa lengo  la kupata fedha mbegu, kwa kuwa mbegu hizo zitazalisha fedha nyingi zaidi kupitia mbegu hiyo”

Semina hiyo iliyowahusisha wanafunzi wa kozi zote chuoni hapo ikiwemo kozi ya uandishi wa  habari, ualimu,sekretari pamoja na kozi ya kompyuta.




picha; baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa kwenye semina leo

Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya mikakati ya kibiashara,  na mada ya huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo bw, Adrea Ngobole.  

Bwana Maygila alisema kuna kuuuza na kununua lakini sio kila mtu anaweza kuuza na kuwataka wote kujenga fikra zao katika kuuza ila waweze kujenga maisha yao
Alisema kama mtu antaka kufanikiwa maishani na kutaka kununua vitu vya thamani ni lazima mtu ajipange vizuri katika  kuuza

“Duniani kuna kuuza na kununua huwezi kukwepa kununua lakini  sio kila mtu anaweza kuuza, unaweza kuuza mawazo, jambo na bidhaa” Alisema Mayagila

Mayagila aliwashauri wanafunzi wake kujiunga   kwenye taasisi za kifedha kwani mkopo ni fedha mbegu na zitawasaidia  kufanikisha biashara zao na kuzaa zaidi
Alihitimisha ufunguzi wa  semina hiyo kwa kusema kwamba ili mtu yeyote afanikiwe ni lazima kusoma vitabu mbalimbali 

“Nyumba isiyyo na vitabu ni mfu, akili isiyopenda kusoma ni mfu pia ,ili uweze kufanikiwa nilazima ulipe gharama za kufanikiwa”

Katika semina hiyo ziliawasilishwa mada kuu tatu na wakufunzi wa chuo hicho, ambapo mwalimu Onesmo Elia Mbise aliwasilisha mada ya mikakati ya kibiashara,  na mada ya huduma kwa wateja iliwasilishwa na bw, Christian Ndege na mada ya Miongozo ya mjasiriamali, iliwasilishwa na Mratibu wa kitengo cha ujasiriamali chuoni hapo bw, Adrea Ngobole.  



  Baadhi ya wakufunzi waliongoza semina;wa kwanza kushoto juu ni Bw. Christian Ndege akifuatiwa na Bw. Onesmo Mbise, Picha kubwa chini ni Bw.Andrea Nobole

 Mwandishi;Benson Mremi

Mhariri;Ckephas ilan