![]() |
Mkuu wa Wilaya ya TANGA, HALIMA DENDEGO |
Mkuu wa Wilaya ya TANGA, HALIMA DENDEGO ametoa ari kwa waandishi wa habari nchini kutumia vyombo vya habari kuwaunga mkono wanawake wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi.
DENDEGO ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ilioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake -TAMWA yenye lengo la kuwahamasisha wanawake kuwania nafasi mbalimbali za uongozia katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao.
Hivi sasa sera ya taifa ni kuwa na Asilimia Hamsini kwa Hamsini katika ngazi za juu za maamuzi.