PATO LA TAIFA LAONGEZEKA

Mkurugenzi wa takwimu za uchumi wa ofisi ya taifa ya Takwimu Morrice Oyuke

Pato la taifa limeongezeka kutokana na ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini. 

Kwa mujibu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu, thamani ya pato la taifa kwa robo ya pili ya mwaka huu wa 2014 imeongezeka na kufikia shilingi tirioni 5.40 kutoka shilingi tirioni 5.05 katika kipindi kama hicho mwaka jana wa 2013. 

Akielezea ukuaji wa pato la Taifa jijini DSM Mkurugenzi wa takwimu za uchumi wa ofisi ya taifa ya Takwimu Morrice Oyuke amesema katika kipindi hicho kasi ya ukuaji wa pato la taifa iliongezeka kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.6 katika kipindi kama hicho mwaka jana. 

Amesema shughuli za mawasiliano, biashara za rejareja na jumla ziliongoza kwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji na shughuli za misitu na uwindaji ziliongoza kwa kuwa na kasi ndogo ya ukuaji katika kipindi hicho.