POLISI WAZUIA MAANDAMANO YA BAVICHA

Kamishna wa Polisi kanda Maalum ya DSM, SULEIMAN KOVA
















Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM limezuia maandamano ya Baraza la Wanawake la CHADEMA-BAWACHA- yaliyopangwa kufanyika siku ya jumamosi, kwa lengo la kumtaka Rais JAKAYA KIKWETE asipokee Katiba inayopendekezwa. 

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi kanda Maalum ya DSM, SULEIMAN KOVA kwa vyombo vya habari jijini DSM, imesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka amri hiyo. 

Taarifa hiyo imesema katika taarifa ya BAWACHA polisi kuhusiana na maandamano hayo, hakuna sababu za msingi kisheria zinazoelezea sababu za Rais kutopokea katiba hiyo. 

Katika hatua nyingine, wakati huu wa kuelekea kwenye siku kuu ya IDD EL HAJ, jeshi la polisi jijini DSM limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi.