Sarafu ya Tanzania yaani shilingi imeanza kufanya vizuri katika soko la fedha baada ya sarafu hiyo kuanza kuimarika dhidi ya sarafu nyingine za kigeni ikiwemo dola ya marekani.
Tathmini ya mwenendo wa biashara katika soko la fedha imeonyesha kuwa sarafu ya Tanzania imebadilishwa kwa tofauti ya shilingi tano dhidi ya dola ya marekani, paundi ya Uingereza na Euro ya Ulaya ambayo ni ya chini ikilinganishwa na ilivyobadilishwa wiki iliyopita.
Katika maduka ya kubadilishia fedha, dola moja ya Marekani imebadilishwa kwa kati ya shilingi 1665 na 1690 za Tanzania , paundi ya uingereza imebadilishwa kwa kati ya shilingi 2680 na 2850 na Euro ya Ulaya imebadilishwa kwa kati ya shilingi 2070 na 2240 za Tanzania.