SERENA WILIAMS AJITOA CHINA OPEN

SERENA WILLIAMS


Mchezaji namba moja kwa ubora DUNIANI katika mchezo wa tenesi SERENA WILLIAMS amejitoa katika mashindano ya wazi ya CHINA kutoka na kuumia goti la kushoto katika mguu wake. 

Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kujitoa katika mashindano nchini CHINA baada kujitoa katika mashindano ya WUHAN kutoka na kuumwa wiki iliyopita. 

Mpinzani wake katika hatua ya mtoani Sam Stosur, ambaye ni bingwa wa mashindano ya wazi ya US mwaka 2011 anatinga moja kwa moja hatua ya robo fainali. 

Pia dada yake mchezaji VENUS amejitoa katika mashindano hayo kutokana na kuugua.