![]() | |
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
|
Kilele cha siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa, hayati mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999 jijini London nchini UINGEREZA ikiambatana na uzimaji mwenge kitaifa baada ya kukimbizwa nchi nzima kwa zaidi ya siku MIA MOJA.
Mwandishi wa TBC ametembelea katika makumbusho ya Taifa jijini DSM na kukutana na watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wakijifunza masuala mbalimbali ya kihistoria.
Katika mazungumzo na wananchi hao waliotembelea kujionea masuala mbalimbali ya kihistoria na kujifunza harakati za ukombozi za Mwalimu NYERERE kwa bara la Afrika baadhi yao wamewataka watanzania kumuenzi baba wa Taifa hayati Mwalimu JULIUS NYERERE kwa kudumisha amani na mshikamano.
Wananchi hao wamesema hayo baada ya kutembelea makumbusho ya Taifa kujionea masuala mbalimbali ya kihistoria na kujifunza harakati za ukombozi za Mwalimu NYERERE kwa bara la Afrika.
Kumbukumbu hizo za kifo cha baba wa Taifa hayati mwalimu JULIUS NYERERE na mbio za mwenge zimehitimishwa kitaifa mkoani TABORA.
Siku hii ya kumbukumbu pia inaenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya vijana.