UN waadhimisha miaka 69 toka kuanzishwa kwake

 

 Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 69 tangu kuanzishwa kwake na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na TANZANIA ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maendeleo na kuishi maisha bora.
Akimwakilisha Rais JAKAYA KIKWETE katika maadhimisho haya jijini DSM Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa ANNA TIBAIJUKA amesema pamoja na mambo mengine TANZANIA itashirikiana na Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo lina athari kwa maendeleo ya nchi.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini ALVARO RODRIGUEZ ameipongeza TANZANIA kwa kudumisha amani na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu na kubeba mzigo wa wakimbizi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini UNA, BENEDICT KIKORE amesema TANZANIA imeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo vijana, kujenga na kusimaia msingi ya haki za binadamu na uwiano sawa wa jinsia katika nafasi za uongozi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka sitini na tisa ya Umoja wa Mataifa ni Hakuna Mtu atakayeachwa nyuma katika kuelekea agenda ya maendeleo ya mwaka 2015.