![]() |
| Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba SAMWEL SITTA |
Akizungumza katika kikao cha bunge la katiba mjini DODOMA, SITTA amesema kila mjumbe ana haki na uhuru wa kutoa maamuzi yake bila kuzuiwa na mtu yoyote.
Aidha Mwenyekiti SITTA amewataka baadhi ya viongozi wa dini kuacha kutumia dini kuchochea uvunjifu wa amani nchini ikiwemo kuwashawishi wananchi kususia mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
Baadhi ya wajumbe wamelaani suala la baadhi ya viongozi wa dini kuingilia masuala ya siasa.
Mjumbe wa bunge hilo OLUOCHI ametaka suala la uhuru na haki kwa vyombo vya habari lipewe kipaumbele katika katiba hiyo, suala ambalo mwenyekiti wa kamati ya uandishi ANDREW CHENGE amesema halina utata.

