Waziri mkuu Mizengo amesema umoja wa kitaifa ndio umesaidia kupata Rasimu ya mwisho ya katiba iliyopendekezwa. Ameongeza kuwa umoja huo ukiendelezwa hakuna kitachoshindikana.
Kauli hiyo ameitoa leo mjini Dodoma akitoa neno la shukrani kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya upigaji kura wa rasimu ya mwisho inayopendekezwa kwa kura za pande zote za muungano. Mh.Pinda ameongeza kuwa wameifikisha katiba katika hatua ya kiukamilifu wakiwa na lengo moja la kujenga Taifa moja na theluthi mbili imepatikana kwa sababu ya umoja.
Kwa upande mwingine Waziri mkuu amesema kwamba ni vema machakato wa Katiba mpya ungemalizika kabla ya Rais ajaye, hivyo kuna haja ya kuhakikisha kuwa jambo hilo linafika mwisho.

