BAO
pekee la mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck
limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa The Hawthorns.
Danny
alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 59 akimalizia mpira uliopigwa na
Santi Cazorla na sasa The Gunners inasogea nafasi ya nne kabla ya
matokeo ya mechi nyingine za wikiendi hii.
Saido
Berahino aligongesha mwamba dakika 10 za mwishoni katika harakati za
kusaka bao la kusawazisha na sasa West Brom inafikisha mechi saba bila
kushinda Hawthorns msimu huu, jambo ambalo lilifanya wazomewe na
mashabiki wao mwishoni mwa mchezo.
Kikosi
cha West Brom kilikuwa: Foster, Wisdom, Dawson, Lescott,
Pocognoli/Gamboa dk74, Mulumbu/Anichebe dk65, Gardner, Dorrans,
Sessegnon/Samaras dk76, Brunt na Berahino.
Arsenal:
Martinez, Chambers, Mertesacker, Koscielny Monreal/Gibbs dk23, Ramsey,
Flamini, Sanchez, Cazorla, Welbeck na Giroud/Oxlade-Chamberlain dk78.

Danny Welbeck akiwa hewani kupiga kichwa kuifungia The Gunners huku kipa Ben Foster akishindwa kuunasa mpita
