![]() |
| Shambulio la bomu lililofanywa kariibu na soko |
Watu 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Wakati umati wa watu wakienda kutoa msaada, mwanamke mwingine alijitoa mhanga.
Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC anasema Wanaigeria wamekosa Imani na jaribio la serikali ya nchi yao kufanya mazungumzo na Boko Haram, kutokana na kuongezeka kwa ghasia hizo.

