![]() |
Freeman Mbowe |
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alisema hayo jana katika
ziara yake ya "Operesheni Delete CCM" alipokuwa akihutubia mkutano Jimbo
la Kasulu na Kibondo mkoani hapa.
Katika kuhitimisha ziara yake Kigoma, alisema kuwa umefika wakati
muafaka kuipumzisha CCM na kuwapa wapinzani ili kuwaletea maendeleo.
Alisema huduma za jamii zimekuwa duni kutokana na uongozi mbovu wa
chama tawala huku mahospitalini kukiwa hamna dawa, pia upande wa elimu
kukiwa na matabaka ya watoto wa wakubwa wakisoma shule za kimataifa na
wale wa maskini wakisoma katika shule za taka ambazo hazina maabara,
vitabu wala walimu wa kutosha.
Operesheni hiyo ilianza mkoani Tabora, Katavi, Kigoma na sasa
itaendelea mkoani Morogoro lengo likiwa ni kuwaelimisha wananchi
kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwachagua wapinzani na
kuikataa katiba iliyopendekezwa.
“Inabidi wana Kigoma kuikataa CCM kuanzia chaguzi za serikali za
mitaa na uchaguzi mkuu ujao kwa kuwachagua viongozi wa Ukawa ili
kuwaletea maendeleo," alisema Mbowe.
CHANZO:
NIPASHE