Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook alikanusha madai ya kumtukana mpinzani wake Lionel Messi na akisisitiza kwamba amewapa go ahead wanasheria wake kufungua kesi dhidi ya mwandishi mwandamizi wa habari za michezo wa Sky Sport, Bleacher Report Guillem Balague.
Jana Jumanne gazeti la Daily Telegraph liliandika habari ya kusisimua kutoka kwenye kitabu cha mwandishi wa SKY Sport Guillem Balague kiitwacho “MESSI”.
Katika kitabu hicho Balague ameandika kwamba:
“Ronaldo, labda ya kwa dalili za kuwa na akili za kitoto ambazo wanazo wacheza soka wengi, anadhani kwamba kuna ulazima kujitamba mbele ya wachezaji wenzie, akionyesha hamuogopi Messi na yupo tayari kushindana nae.
“Ndio maana, kwa mujibu wa baadhi ya wachezaji wa Real Madrid, CR7 amekuwa akimpa Messi majina ya ajabu kwa kumuita ‘motherf—-r’; na pale anapomuona mchezaji yoyote wa Real Madrid akiongea na Leo Messi, basi nae huishia kumuita (tusi) ‘motherf—-r’.”
Taarifa hii ya Balague ilitengeneza vichwa vya habari vingi kwenye media na haikumchukua Ronaldo muda mrefu kujibu shutuma hizo kupitia mashabiki wake millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook.
Pamoja na kukanusha taarifa kumtukana Messi – Ronaldo amesisitiza kwamba amewapa wanasheria wake ruhusa ya kuchukua hatua za kisheria juuya mwandishi huyo, huku akisema kwamba anawaheshimu wanasoka wote na Messi akiwemo.
