
Viongozi wa mataiifa ya magharibi
wanaohudhuria mkutano wa mataifa tajiri, G-20 mjini Brisbane, Australia,
wameionya Urusi ifuate makubaliano ya kusitisha mapigano Ukraine, ama
sivyo itakabili vikwazo zaidi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David
Cameron, alimwambia Rais Putin kuwa uhusiano baina ya Ulaya na Urusi
utabadilika iwapo wanajeshi wa Urusi watabaki Ukraine.Rais Obama alisema hatua za Urusi zinachusha.
Urusi inakanusha kuwa ina wanajeshi wake ndani ya Ukraine.
Msemaji wa Bwana Putin alitoa maanani ripoti kuwa kiongozi wa Urusi anapanga kuondoka mapema kwenye mkutano.
