GUINESS YAWAKUTANISHA MWANAUME MREFU NA MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI

Alhamis ya jana (November 13) mwanaume mrefu kuliko wote duniani na mfupi kuliko wote walikutana katika tukio lililofanyika London ambapo walipiga picha ya pamoja wakipeana mikono.

Tukio hilo lilikuwa ni lakumi la mwaka la rekodi za Guinness kusherehekea rekodi zilizowekwa na dunia. Guiness waliwasafirisha wanaume hao ambao ni Sultan Kosen kutoka uturuki (Mrefu) na Chandra Bahadur Dangi  (mfupi) kutoka Nepal kwaajili ya picha ya kipekee.



Kosen (31) ni mkulima wa msimu mwenye urefu wa feet 8na nchi 3, ana uwezo wa kushika kikapu cha goli la bascket bila kuruka, alishika rekodi hiyo mwaka 2009 baada ya kumpita urefu Xi Shun wa China mwenye feet 7 na nchi 9



Dangi (74) yeye ana urefu wa nchi 21½ na ni mwanaume mfupi aliwahi ku-rekodiwa na Guiness na ana uzito wa Pound 32