GURDIOLA AMFAGILIA MESSI ASEMA REKODI YAKE ITADUMU MIAKA 600

Aliewahi kuwa Manager wa Barcelona Pep Guardiola,ammwagia misifa Lionel Messi baada ya kuvunja rekodi ya kufunga magoli mengi La Liga na kudai kuwa itachukua miaka 600 mtu mwingine kuja kuvunja rekodi hiyo.
 
 Messi alitandika Hat-trick weekend iliyopita na kuvunja record iliyowekwa na Telmo Zarra (251)  miaka 60 iliyopita kwenye kitabu cha rekodi kwa kufikisha magoli 253 kwenye La Liga.


Messi alifikisha magoli 251 jumamosi iliyopita dakila ya 21 Barcelona ilipokuwa ikicheza na Sevilla na kufikia record ya Zarra, na akaivunja record hiyo ndani ya dakika ya 72 kwa kuingeza goli la pili na kumaliza hat-trick katika ushindi wa 5-1.

Guardiola, ambae alishafanya kazi na Messi kati ya mwaka 2008 na 2012 amewataka watu kumpa hongera Messi kwa alichokifanikisha kwa kuwa amevunja record ambayo haikutegemewa kuvunjwa