HAKUNA WA KULIZUIA BUNGE KUJADILI ESCROW

Tue Nov 25 2014
Spika wa Bunge ANNE MAKINDA
 
Spika wa Bunge ANNE MAKINDA amesema hakuna mtu anayeweza kulizuia bunge kutekeleza kazi zake na hivyo kuwataka wabunge kutokuwa na hofu ya kupewa fursa ya kujadili ripoti ya CAG kuhusiana na kashfa ya Escrow.

Akijibu mwongozo bungeni Mjini DODOMA Spika MAKINDA amesema kwa mujibu wa taratibu za bunge, kamati iliyopewa kazi ya kushughulikia ripoti ya CAG inapaswa kumwandikia Spika barua kumtaarifu kuwa imekamilisha kazi yake, ili muswada huo upate fursa ya kujadiliwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Spika, anachosubiri sasa ni taarifa ya kamati kama imekamilisha kazi hiyo ili aweze kuipanga kujadiliwa.


Katika hatua nyingine Waziri wa Fedha SAADA MKUYA amewasilisha bungeni muswada wa sheria ya kodi ya ongezeko la thamani wa mwaka 2014