Baba mdogo wa marehem Geez Mabovu (30) amesema kuwa Mbovu ambae
amefikwa na mauti jana usiku majira ya sa mbili na dakika 15 alikuwa
anasumbuliwa na kifua na kufariki akiwa nyumbani kwao
"Mimi naitwa Abasi Upete ni baba yake mdogo na Geez Mabovu, actually
katikati hapa madaktari kifua kilikuwa kinamsumbua kwahiyo walikuwa
wanashindwa kujua tatizo ni nini, maana amefia nyumbani tu kwahiyo
wakasema hawawezi kufanya chochote mpaka
waweze kupata makohozi ili tuweze kujuwa kifua
kulikuwa kinamsumbua hasa ni nini kama ni kifua kikuu au tatizo gani
lakini bahati mbaya ndio amefariki saa mbili na dakika kumi na tano.
ni
kama wiki mbili na nusu zilizopita hivi hali ilizidi kuwa mbaya katikati
hapa lakini kaka yangu ambae ni baba yake alienda kumchukua Daresalaam
kama wiki mbili na nusu hivi, tutakuwepo mlandege karibu na tenki la
maji, ana miaka 30, mpaka sasa hivi hatujapata taarifa zozote unajua
vijana hao, na mazishi yatakuwepo saa kumi tutasalia katika msikiti wa
mwangata maeneo ya mololo" amesema baba yake mdogo