
Kiongozi wa mpito nchini BURKINAFASO ametupilia mbali tamko la UMOJA wa AFRIKA la kukabidhi madaraka kwa raia nchini humo.
Luteni Kanali ISAAC ZIDA amezungumza na viongozi wa vyama vya upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali na kuwaambia kuwa haogopi vikwazo vya AU.
Amesema kuwa nchini BURKINAFASO wamekubaliana kufanya uchaguzi mwaka ujao na sio nani ataongoza nchini hiyo mpaka siku ya uchaguzi.
Jeshi lilichukua madaraka nchini BURKINAFASO baada ya rais BLAISE COMPAORE kulazimishwa kuondoka madrakani baada ya maandamano makubwa yaliyopinga uongozi wake.