LICHA ya kusema kuwa anataka abaki
Barcelona milele lakini Lionel Messi ameacha mlango wazi kuihama baada
kudokeza upo uwezekano wa kuhama baada ya Msimu huu. Messi, ambae sasa ni Nahodha wa Argentina na ambae amewahi kuwa
Mchezaji Bora Duniani mara 4, alijiunga na Chuo cha Soka cha Barca akiwa
na Miaka 13 na kudumu hapo hadi sasa.
Lakini Messi, mwenye Miaka 27 sasa, amekuwa na kiwango hafifu kwa
kipindi cha Miezi 18 akikumbwa majeruhi ya mara kwa mara na pia kupatwa
na misukosuko ya kuburuzwa Mahakamani yeye na Baba yake Mzazi huko Spain
akidaiwa kukwepa kulipa Kodi.
Msimu uliopita Barca ilitoka kapa bila kutwaa Taji kubwa na Msimu huu
wapo Nafasi ya Pili kwenye La Liga wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Real
Madrid baada ya Mechi 11 za Ligi.
Kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, Barca wameshafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Tumu 16 huku wakiwa na Mechi 2 za Kundi lao mkononi.
Ikiwa Messi atapelekwa Sokoni kuuzwa basi Dau lake linakadiriwa litakuwa si chini ya Euro Milioni 100