LIVERPOOL imelazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Wenyeji,
Ludogorets walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Dani Abalo dakika
ya tatau, kabla ya Liverpool kusawazisha kupitia kwa Rickie Lambert
dakika ya nane.
Wekundu
wa Anfield walipata nao lililoelekea kuwa la ushindi kupiti kwa Jordan
Henderson dakika ya 37 kabla ya Georgi Terziev kuisawazishia Ludogorets
dakika ya 88.
Kikosi
cha Ludogorets kilikuwa; Stoyanov, Junior Caicara, Moti, Terziev,
Minev, Misidjan, Dyakov, Fabio Espinho/Younes dk80, Mihail
Aleksandrov/Wanderson dk72, Marcelinho na Dani Abalo/Quixada dk69.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Toure, Manquillo, Henderson, Gerrard, Lucas, Lambert, Allen na Sterling/Moreno dk82.

Wachezaji
wa Liverpool, Steven Gerrard na Rickie Lambert wakiwa wanyonge baada ya
George Terziev (hayupo pichani) kuisawazishia Ludogorets