MACHINGA COMLEX YATEKETEA KWA MOTO VYUMBANI


 
MACHINGA COMPLEX
 
Baadhi ya vyumba katika jengo la wafanyabiashara ndogo ndogo la MACHINGA COMPLEX jijini DSM vimeteketea kwa moto.

Kwa mujibu wa Christina Lyabonga kutoka Jeshi la zimamoto Ilala waliarifiwa kutokea kwa moto huo majira ya saa saba nchana na kuwasili katika eneo hilo muda mfupi nakukuta wananchi wameshaanza kuzima moto huo kwakutumia vifaa maalum vya kuzimia moto (FIRE EXTINGUISHER)

Mmoja wa wafanyabiashara aliyeathirika na moto huo IDD JUMA amesema moto huo umeenea katika ofisi yake baada ya kuwaka katika eneo la kizimba cha jirani yake na kuteketeza stakabadhi za bima

Mpaka sasa bado hasara iliyosababishwa na moto huo haijajulikana