Manchester United imeripotiwa kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona
na timu ya taifa ya Hispania Victor Valdez baada ya kufanya nae mazoezi
kwa muda wa karibu mwezi mzima .
Valdez ambaye aliihama Barcelona baada ya mkataba wake kuisha msimu
uliopita alikuwa karibu kujiunga na klabu ya Liverpool lakini jeraha
baya la goti alilopata katikati ya msimu uliopita lilizuia usajili wake
kwenda Anfield.
Victor Valdez yuko mbioni kukamilisha usajili wake na Manchester United .
Katika kipindi hiki kocha wa Manchester United Louis Van Gaal alimpa
kipa huyo nafasi ya kufanya mazoezi na United hali ambayo ilimuweka
karibu na usajili ndani ya klabu hiyo .
Usajili wa Valdez ulithibitishwa na kipa namba moja wa United David
De Gea ambaye alizungumza na waandishi wa habari na kuwathibitishia kuwa
United imemsajili Valdez.
De Gea aliwaambia waandishi kuwa United haijamsajili Valdez kama mbadala wake.
De Gea alikuwa akijibu maswali ya waandishi walimhusisha na usajili
kuelekea Real Madrid na katika kukanusha kwake taarifa hizo De Gea
aliwaambia waandishi wa habari kuwa Valdez hajasajiliwa kama mrithi wa
nafasi yake .