Mtoto wa
kwanza wa mchezaji wa zamani wa Manchester United Beckham na
mwanamitindo Victoria amesign kuichezea timu ya mpira wa miguu "Arsenal"

Brookyln
(15)aliyewahi kufanya mazoezi na klabu hiyo ya London amekataa kufuata
nyayo za mzazi wake na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu
hiyo licha ya fuatiliwa kwa karibu na klabu kama Chelsea na Manchester United.
Gazeti la The Daily Star
lilifichua kuwa Brooklyn amesaini mkataba wa awali wa mwaka mmoja baada
ya kuwafurahisha makocha wa klabu hiyo wakati wa mazoezi aliyofanya
klabuni hapo hivi karibuni.
Inadaiwa kwamba Arsenal wamekuwa wakimfuatilia chipukizi huyo kwa muda mrefu na wapo tayari kumpa mkataba wa muda mrefu, endapo ataendelea kung’ara msimu huu.
Inadaiwa kwamba Arsenal wamekuwa wakimfuatilia chipukizi huyo kwa muda mrefu na wapo tayari kumpa mkataba wa muda mrefu, endapo ataendelea kung’ara msimu huu.
Chanzo cha
habari kilichonukuliwa na The Daily Star kimefichua kuwa Brooklyn ni
kijana mwenye kipaji kikubwa , ameonyesha ukomavu na utulivu kwenye
mazoezi, hata mechi za timu ya watoto ambazo amekuwa akichezeshwa.
Watoto wa Beckham wamekuwa sehem ya Arsenal kwa
miaka sasa huku Romeo mwenye miaka 12 kwa sasa anachezea arsenal kwa
wenye umri chini ya miaka 13, na Cruz (9) anachezea team ya wenye miaka
chini ya miaka 10, club iko London na Beckham ni rafiki wa manager wa
Arsenal, Arsene Wenger.