NCHI ZA ULAYA ZAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KUMALIZIKA VITA YA DUNIA

Nchi za ulaya zaadhimisha kumbukumbu ya kumalizika vita kuu ya kwanza ya dunia

Nchi mbalimbali katika bara la ULAYA,jana zimeadhimisha kumbukumbu ya kumalizika kwa vita kuu ya kwanza ya dunia.
Wadau mbalimbali wa nchi za UBELGIJI na UFARANSA, ambako vita hivyo vilipiganwa sana na watu wengi kupoteza maisha, wamekutana kukumbuka vita hivyo.

Nchini UFARANSA rais FRANCOIS HOLLANDE, amezindua kumbukumbu nyingine ya vita hivyo nchini mwake.

Kumbukumbu hiyo inajumuisha askari kutoka mataifa zaidi ya 40 duniani yaliyoshirikiana na UFARANSA wakati wa vita hivyo.

Nchini UINGEREZA kumbukumbu ya kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia imekuwa ya aina yake, kwa kijana askari mwenye umri wa miaka 13 kuweka ua la kumbukumbu ya kumalika kwa vita hivyo. Hatua hiyo ni kuwakumbuka askari waliopoteza maisha yao wakipigania taifa lao.