RAIS KIKWETE AFANYIWA UPASUAJI MAREKANI

Photo: Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho
Kikwete alifanyiwa upasuaji wa
tezi dume (prostrate) katika
Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la
Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Ikulu ya
Tanzania, Rais Kikwete
amefanyiwa upasuaji huo baada
ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake
kujiridhisha kuwa Rais alikuwa
anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi
cha saa moja unusu ambapo
inaelezwa kuwa umefanyika
salama na kwa mafanikio
makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais
Kikwete inaendelea vizuri japo
bado yuko wodini akiendelea
kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
.
  
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.

Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.