RAIS WA IRAN |
.
Rais Rouhani ameyasema hayo Jumamosi mjini Tehran wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Rafael Ramirez.
Rais wa Iran pia amesisitiza umuhimu wa mashauriano baina ya Iran na Venezuela kuhusu masuala muhimu ya uchumi wa dunia kama vile uthabiti wa bei ya mafuta.
Matamshi ya Rouhani yanakuja huku kukitazamiwa kufanyika kikao cha 166 cha mwaziri wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi Duniani OPEC.
Kikao hicho kitakachofanyika Novemba 27 kitajadili kushuka kwa kasi bei ya mafuta ya petroli duniani.
Wakati huo huo Waziri wa Mafuta Iran Bijan Namdar Zangane amesema ni vigumu kwa bei ya mafuta kupanda tena katika mustakabali wa karibu.
Akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, amesema nchi za OPEC zinapaswa kushirikiana ili kuleta uthabiti katika soko la mafuta.
Nchi za OPEC zinazalisha takribani asilimia 40 ya mafuta yote ya petroli duniani huku Iran ikiwa ya tatu katika uzalishaji.
Wanachama wa OPEC ni pamoja na Algeria, Angola, Ecuador, Iran, Iraq, Libya, Kuwait, Nigeria, Qatar, Saudi Arabia, the Umoja wa Falme za Kiarabu, na Venezuela.