BAO
pekee la Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo limeipa ushindi wa
1-0 ugenini Real Madrid dhidi ya FC Basle katika mchezo wa Kundi B Ligi
ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Mreno
huyo, aliyeondoka Manchester United kutua Madrid kwa dau la rekodi,
alifunga bao hilo pekee muhimu dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya
Mfaranda, Karim Benzema.
Real
Madrid sasa inaongoza Kundi B kwa rekodi nzuri ya ushindi, huku ikiwa
imesaliwa na mecni moja, wakati kwa kipigo cha leo, Basle hatima yao
itajulikana baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Liverpool kama watasonga
mbele au, la.
Kikosi
cha Basle kilikuwa; Vaclik, Degen/Hamoudi dk76, Schar, Suchy, Safari,
Elneny, Frei/Diaz dk83, Zuffi/Kakitani dk87, Gonzalez, Embolo na Gashi.
Real
Madrid: Navas, Arbeloa, Varane, Ramos, Coentrao, Kroos, Isco/Nacho
dk93, Rodriguez/Marcelo dk89, Bale, Ronaldo na Benzema/Illarramendi
dk71.

Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid

Gareth Bale wa Real Madrid akipambana na beki wa Basle, Philipp Degen