Aliyekuwa
mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya
kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na
kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya
kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.