
Kabla ya Mechi kuanza, Rooney alikabidhiwa Kofia ya Dhahabu na Sir Bobby Charlton ikiwa ni Tuzo kwa kuichezea England Mechi 100.
Hadi Mapumziko, Bao zilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili Dakika ya 57 Jordan Henderson alijifunga mwenyewe kwa Kichwa kufuatia Frikiki na kuwapa Slovenia uongozi lakini Dakika 2 baadae Rooney aliisawazishia England kwa Penati baada ya yeye mwenyewe kukwatuliwa na Bostjan Cesar.
Danny Welbeck alifunga Bao 2, Dakika za 66 na 72, na kuipa England ushindi wa Bao 3-1.
Ushindi huu umeifanya England ipae kileleni ikiwa na Pointi 12 ikifuatiwa na Lithuania na Slovenia zenye Pointi 6 kila moja.
