![]() |
| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo tawi la Tanzania MIKE SEO |
Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Sumsung ya Korea inatarajia
kufanya uzinduzi wa toleo jipya la simu ya Samsung Galaxy Note 4 nchini
Tanzania katikati ya mwezi huu.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo tawi la Tanzania MIKE SEO, uzinduzi wa simu hiyo unafanyika hapa nchini baada ya kuonekana Tanzania inasoko kubwa la simu za kiganjani.
Simu ya Galaxy Note 4 imetengenezwa kwa fremu ya chuma na inamfumo wa kutunza chaji ambao unaruhusu kuhifadhi chaji kwa ajili ya matumizi muhimu ya simu pale chaji inapoisha kabisa.

