
Andre Schurrle, Mjerumani wa Miaka 24 ambae alisainiwa na Chelsea Miezi 18 iliyopita kutoka Bayer Leverkusen, amekuwa hayuko kwenye fomu nzuri tangu arejea kutoka Brazil alikoisaidia Germany kutwaa Kombe la Dunia na hali hiyo imesababisha uvumi kuwa atauzwa Mwezi Januari.
Lakini Schurrle mwenyewe ameibuka Mtandaoni na kudai bado ana Mwaka mmoja na Chelsea na kuuzima uvumi huo.
Msimu huu, Schurrle amecheza Mechi mbili tu kwa Dakika zote 90, zote za Capital One Cup, na mara nyingi Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amemtaka Mchezaji huyo kuongeza bidii.