SOUTH AFRICA NA CAMEROON ZAINGIA FAINALI AFCON, UGANDA YAITUNGUIA GHANA KAMPALA

JANA, South Africa na Cameroon zimeungana na Algeria, Cape Verde na Tunisia kutinga Fainali za AFCON 2015 zitakazochezwa huko Equatorial Guinea kuanzia Januari 17.
 
South Africa, wakicheza Mechi yao ya kwanza tangu kuuliwa kwa Nahodha wao na Kipa wao Senzo Meyiwa, wameichapa Sudan Bao 2-1 na kufuzu kucheza Fainali toka Kundi A wakiwa na Mechi 1 mkononi ambayo watamaliza Ugenini na Nigeria Jumatano Novemba 19.

Bao za South Africa zilifungwa na Thulani Serero na Tokelo wakati la Sudan liliingizwa na Salah Elgazoli.

Nao Nigeria wamejiweka hai kutinga Fainali baada ya kuifunga ugenini Congo Bao 2-0 kwa Penati ya Dakika ya 59 ya Uche Nwofor na Bao la mwishoni la Aaron Samwel alieingizwa Dakika za mwishoni.

Nigeria sasa wapo Nafasi ya Pili licha ya kufungana Pointi na Congo waliowazidi kwa ubora wa Magoli.

Bao la Dakika ya 10 la Savio Kabugo limewapa Uganda ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Ghana huko Kampala kwenye Mechi ya Kundi E la AFCON 2015


NCHI ZILIZOFUZU KUINGIA FAINALI:

-MWENYEJI: Equatorial Guinea

-KUNDI A: South Africa,

-KUNDI B: Algeria,

-KUNDI C:

-KUNDI D: Cameroon,

-KUNDI E:

-KUNDI F: Cape Verde,

-KUNDI G: Tunisia,

**Kila Kundi kutoa Timu 2 na Timu ya 15 ni Mshindi wa Tatu Bora mmoja toka Kundi lolote.

**FAINALI kuchezwa kuanzia Januari 17 hadi Februari 8