
Wimbo
mpya kabisa wa Yomoto Band ambao ndani yake ameshirikishwa mkali wa
masauti Christian Bella, umevuja kabla hata haujakamilika na tayari
umesambaa kinoma kwa wadau wa muziki.
Hata
kabla haujafanyiwa mixing na kupekekwa radioni, wimbo huo ukavuja na
katika hali isiyotarajiwa na bila kujali ubora wa kazi, mashabiki
wakaanza kutumiana wimbo huo kwenye simu zao kupitia mtandao wa Whatsapp
na kuenea kila kona hadi kwa watu wa bodaboda.
Ngoma
hiyo iliyopewa jina la “Rubani wa Moyo” inatisha kwa utamu, imejaa
mistari mitamu ya mapenzi huku Bella na madogo wa Yamoto wakifunikana
ile mbaya kwenye kutuma masauti.