CAG MPYA KUFANYA MAREJEO KWENYE KESI YA TEGETA ESCROW

Prof MUSSA JUMA ASSAD
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG -Prof MUSSA JUMA ASSAD, ameahidi kufanya marejeo katika Ripoti ya ofisi yake kuhusu Akaunti ya TEGETA ESCROW ambayo iliibua mjadala mzito Katika Mkutano wa Kumi na sita na Kumi na saba wa bunge wiki iliyopita mjini DODOMA.

Prof ASSAD ameeleza hayo mjini ARUSHA baada ya kufungua Mkutano wa Bodi ya wahasibu NBAA ambapo amesema katika ripoti hiyo ya TEGETA ESCROW kuna mambo machache yanayohitaji kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya NBAA, Profesa ISSAYA JAILO, amesema wahasibu na wakaguzi wakuu wa hesabu ni vema wakafahamu umuhimu wa masuala ya mafuta ,gesi pamoja na utalii ambayo ndiyo chanzo cha uchumi mkubwa kwa Taifa, huku Taasisi na mashirika yaliyofanya vizuri katika hesabu zake yakazawadiwa tuzo mbalimbali