VINARA wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumatano Usiku wameichapa Tottenham Bao 3-0 na kuendelea kupaa kileleni mwa Ligi hiyo.
Bao za Chelsea zilifungwa na Eden Hazard, Didier Drogba na Loic Remy.
Nao Arsenal wameitungua Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 89 la Alexis Sanchez.
Mabingwa Watetezi Man City wameichapa Sunderland Bao 4-1 kwa Bao za
mbili za Sergio Aguero, Jovetic na Zabaleta huku Bao la Sunderland
likifungwa na Wickham.
Everton na Hull City zilitoka Sare ya Bao 1-1 wakati Romelu Lukaku
alipotangulia kuifungia Everton na Sone Aluko kuisawazishia Hull Hull
City.