DIAMOND NA WEMA WARUDIAN TENA.....soma zaiidii hapa


UNAJIMU! Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Shehe Yahya amesema kuwa, penzi la mastaa wa Kibongo,Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ bado halijafika mwisho, watarudiana na kufunga ndoa.

Akizungumzia penzi la wawili hao ambao siku chache zilizopita wameripotiwa kumwagana alisema, hali hiyo ni ya mpito tu haimaanishi kuwa hiyo ndiyo tamati ya mapenzi yao, sababu nyota zao zinategemeana japo ya Wema ina nguvu kubwa kuibeba ya Diamond.

Msifikiri kwamba penzi lao ndiyo limefika mwisho, hakuna kitu kama hicho ni mara ngapi wameachana na kurudiana hata hili la sasa natabiri watarudiana,” alisema Malim.
Credit GPL