DORTMUND YABURUZA MKIA MTAWALIA BUNDASLIGA

Mon Dec 01 2014

DORTMUND yashika mkia BUDASLIGA
NCHINI UJERUMANI katika BUNDESLIGA, BORUSSIA DORTMUND imejikuta mkiani mwa ligi hiyo,baada ya kufungwa mabao mawili kwa bila na EINTRACHT FRANKFURT.

Mabao ya FRANKFURT yamefungwa na ALEXANDER MEIER na HARIS SEFEROVIC,na Wolfsburg imeifunga BORUSSIA MÖNCHENGLADBACH bao moja kwa bila lilofungwa na ROBIN KNOCHE.

Mabingwa hao wa ujerumani wa msimu wa 2011 na 2012,wamepoteza mechi tisa kati ya michezo 13 waliocheza msimu na kujikusanyia ALAMA 11 na hivyo kusababisha kocha Klopp kuwa katika pressure kubwa ya kutimuliwa kazi.

BAYERN MÜNCHEN inaongoza BUNDESLIGA ikiwa na ALAMA 33, WOLFSBURG inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 26,na BAYER LEVERKUSEN ipo katika naafsi ya tatu ikiwa na alama 23.