![]() |
| Shughuli za mazishi hufanywa kwa makini kuepuka maambukizi ya Ebola |
Maafisa wa Afya nchini Sierra Leone
wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya mgodi wa Almasi, na kusababisha
hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola haujaripotiwa ipasavyo.
Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.
Sierra Leone ina idadi kubwa zaidi ya Watu wenye Ebola Afrika Magharibi, ikiwa na Watu walioathirika 7,897 tangu kuanza kwa ugonjwa huo.
WHO imesema katika kipindi cha takriban siku 11 mjini Kono, Miili 87 ilizikwa.
Miili ya Watu waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola ni hatari kwa maambukizi hivyo huzikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

