Baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha katika michuano ya ndani
na nje ya nchi yao – klabu ya Liverpool leo imejitupa uwanjani kucheza
na timu iliyowapa kipigo kizito Man United – klabu ya Leicester City.
Mchezo huo wa Barclays Premier League uliochezwa katika dimba la
Leicester City umemalizika kwa Liverpool kuwatafuna Leicester 3-1.
Magoli ya Adam Lallana, Steven Gerrard na Jordan Henderson yalitosha
kuwapa pointi 3 Liverpool na kuwafanya sasa kutimiza pointi 20 katika
msimamo wa ligi kuu ya England