Rais wa KENYA, UHURU KENYATTA
Hapo jana ICC ilitoa muda wa wiki moja kwa waendesha mashtaka wa korti hiyo waamue iwapo wataendelea na kesi dhidi ya Rais UHURU KENYATTA wa Kenya au kuondoa mashtaka dhidi yake.
Mahakama hiyo ilimtaka FATOU BENSOUDA Mwendesha Mashtaka mkuu wa mahakama hiyo atoe ushahidi dhidi ya Rais wa Kenya la sivyo aondolewe mashtaka yanayomkabili.
Mahakama hiyo ilisema kuwa, kucheleweshwa kwa kesi ya UHURU KENYATTA ni kinyume na maslahi na haki.
Waendesha mashtaka wa mahakama hiyo wamesema kuwa UHURU anayetuhumiwa kuhusika katika jinai za baada ya uchaguzi mkuu nchini KENYA mwaka 2007, ametumia uwezo wake wa kisiasa kuzuia uchunguzi wao, hasa baada ya kuwa Rais mwaka uliopita.