JUVENTUS KIBIBI KIZEE CHA TURIN YAJIKITA KILELELNI




JUVENTUS yajikita kileleni Serie A
MABINGWA wa ITALIA, JUVENTUS, imeendelea kujikita kileleni mwa Serie A baada ya kuibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa MOJA na TORINO.
Mabao ya JUVE yamefungwa na ANDREA PIRLO na ARTURO VIDAL wakati bao la kufutia machozi limefungwa na BRUNO DA SILVA.

Ushindi huo wa 11 wa JUVE unatanua pengo la alama dhidi ya ROMA inayoshika nafasi ya pili na kufika hadi ALAMA SITA, ROMA imeibuka na ushindi mabao MANNE kwa MAWILI dhidi ya INTER MILAN inayoongozwa na kocha ROBERTO MANCINI.

Matokeo ya michezo mingine,Cagliari ikiwa nyumbani imefungwa mabao MANNE kwa mtungi na FIORENTINA na Cesena imefungwa mabao MATATU kwa BILA na Genoa.

Palermo imechapa Parma mabao MAWILI kwa MOJA, EMPOLI imetoka suluhu na ATALANTA,AC MILAN ikaitandika UDINESE mawili kwa BILA.
MSIMAMO wa Serie A, Juventus inaongoza ikiwa na AALAMA 34,Roma ya pili na ALAMA 31,Genoa inashika nafasi ya tatu ikiwa na ALAMA 23 na Napoli ya nne ikiwa na ALAMA 22.