Show ya Jahazi iliyoruka siku ya jana December 10 kulikuwa na ugeni kutoka Shirika la Utangazaji Uingereza BBC ambapo Mtangazaji Salim Kikeke alikuwepo kwa ajili ya mahojiano kwenye kipindi hicho.
Aliaanza kwa kuelezea kuhusu namna ambavyo BBC wanapata habari kutoka maeneo mbalimbali duniani; “Shirika
la Utangazaji la BBC kimataifa ndio lenye waandishi wa habari wengi
zaidi Duniani kuliko shirika lolote la habari la Kimataifa.. Kitu
kikitokea kokote Duniani lazima hiyo taarifa tutakuwa nayo…”– Salim Kikeke.
Kikeke ameelezea namna ambavyo BBC wanaandaa habari; “Unavyojitayarisha
nusu saa kabla ya kwenda hewani huwa tunafanya rehearsal jambo ambalo
nakumbuka wakati tuko hapa Tanzania tulikuwa hatulifanyi na hata
ukiwaambia watu wanasema kwanini ufanye rehearsal wakati umeshazoea…”
Mtangazaji huyo alitoa pongezi kwa kituo cha Clouds FM kutimiza miaka 15; “Nilitaka
kutoa pongezi sana za kufikisha miaka 15 ya Clouds kutoa burudani na
habari… Inanikumbusha mbali sana kwa sababu wakati Clouds inaanza tukiwa
mtaani bado tunasikia kwamba jamani kuna redio mpya inakuja na ilikuwa
kati ya redio za mwanzo mwanzo kabisa za FM…”– Salim Kikeke.
Hapa alizungumza kuhusu kitu kinapaswa kuzingatiwa zaidi kwenye uandishi wa habari; “Kinachozingatiwa
zaidi ni misingi ya uandishi wa habari na ndiyo ya kuifuatilia kwa
umakini.. Kama kuna taarifa imetoka na unaibeba hivyo hivyo bila ya
kuithibitisha na bila ya kuitafuta upande wa pili unasemaje kuhusu
taarifa hiyo… hicho ni cha kuzingatia kwa mwandishi wa habari yoyote…
Kitu ambacho tunajisahahu ni kutokusoma, hatusomi kwa makini kufuatilia…
Ukijitahidi kusoma kila kinachowezekana unakuwa taarifa unaifahamu…”– Kikeke.
Akiisimulia safari yake ya kwanza kufika Uingereza kwa ajili ya kuanza kazi na BBC, Kikeke amesema; “Nilipofika
London, Tido Mhando ndio alikuwa Mkurugenzi pale, nilipofikia kwenye
Hotel akanipigia simu na kusema kama nimewasili kesho niende kazini…“
Kuhusu malengo ya Dira ya Dunia, Kikeke amesema; “Katika
zile wiki mbili za mwanzo ambazo nimekaa Tanzania nimeshafanya stori
mbili… Nilienda Pemba.. Dira ya Dunia tulipoanza tulisema pamoja na kuwa
tutakuwa tukiyataja kwa kuwa kama kuna vita unasema.. Sisi tumeweka
ahadi kwamba tutatangaza habari nzuri ambazo zipo katika maeneo yetu…”