Luis Enrique
BUSQUETS alifunga bao hilo,baada ya kipa wa VALENCIA, DIEGO ALVES kuokoa mpira wa kichwa wa NEYMAR,akimalizia krosi ya MESSI, na kwa ushindi huo, BARCA imepunguza pengo na kufika ALAMA MBILI,nyuma ya vinara REAL MADRID.
Katika mchezo huo,LIONEL MESSI ilibidi atibiwe baada ya kupingwa na chupa ya PLASTIKI na mashabiki wa VALENCIA, katika dimba la MESTALLA.
Matokeo ya michezo mingine CÓDOBA imefungwa mabao MAWILI kwa BILA na VILLARREAL, SEVILLA imeichapa GRANADA mabao MATANO kwa MOJA na ATLÉTICO DE MADRID imeibuka na ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA dhidi ya DEPORTIVO DE LA CORUÑA.
REAL MADRID inaongoza LA LIGA ikiwa na ALAMA 33, BARCELONA inashika nafasi ya pili akiwa na ALAMA 31, ATLÉTICO DE MADRID inashika nafasi ya tatu ikiwa na ALAMA 29
