MATUKIO YA AJALI YA BASI LA MOHAMED TRANS ILIYOTOKEA IGUNGA.

MATUKIO YA AJALI YA BASI LA MOHAMED TRANS ILIYOTOKEA IGUNGA.

Basi la kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali mbaya Igunga ambapo watu saba wanadaiwa kupoteza maisha maisha.
Inadaiwa kuwa mbali na kuua pia abiria wengi wamejeruhiwa baada ya basi hilo  la Mohammed Trans kukatika 'steeering power' likaacha njia na kupinduka huku kukiwa na taarifa kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kugonga shimo 

  Basi hilo limepinduka leo majira ya saa nane mchana, ambapo maiti na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Picha zote zikionyesha mandhari ya sehemu ajali hiyo ilipotokea.